Back to top

Awamu ya kwanza mazishi ya maiti zilizoharibika kwa moto kuzikwa leo.

11 August 2019
Share

Awamu ya kwanza ya mazishi ya maiti zilizoharibika kwa moto kuzikwa leo majira ya saa 10 jioni kwenye makaburi ya Kola yaliyopo manispaa ya Morogoro.


Hayo yamesemwa  na  Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera,bunge ,ajira na watu wenye Ulemavu Mh Jenister Muhagama wakati akiongea na waandishi wa Habari katika hospitali ya rufaa mkoani Morogoro.

Majeruhi 12 ambao hali zao ni mbaya wamesafirishwa jana usiku  kuelekea hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu zaidi.


Kwa ujumla mpaka muda huu idadi ya waliopoteza maisha katika ajali ni 64 na majeruhi 70.