Back to top

Aweso aagiza kufukuzwa kazi wasimamizi wa miradi ya maji Bunda

14 September 2021
Share

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kuwafukuza kazi wasimamizi wa Mradi wa maji wa Nyabeho Wilayani Bunda na Mradi wa Mgango Kiabakari kwa kushindwa kusimamia miradi hiyo kiufasaha na kuleta wasimamizi wengine wenye dhamira ya dhati ya kufanya kazi.

Aweso ameyasema hayo wakati alipotembelea miradi hiyo na kukuta wasimamizi hao hawapo maeneo yao ya kazi.