
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso anamwakilisha Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji unaofanyika Umoja wa Mataifa, New York, tarehe 22-24 Machi 2023.
Waziri Aweso amehutubia Mkutano huo jana jioni ambapo Katika hotuba yake amebainisha umuhimu wa dunia kukaa pamoja na kusimamia agenda ya maji, thamani ya maji katika maisha na uchumi, kuongeza uwekezaji katika eneo la maji, ushirikiano wa kimataifa katika maji, pamoja na utafutaji wa fedha kwa ajili ya maji.
Aidha, Katika mkutano, Tanzania imebeba agenda mbili ambazo ni utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji Awamu ya Tatu (Water Sector Development Programe III) ambayo inahitaji Dola za Marekani Bilioni 6.47 katika kipindi cha 2022-2025.