Back to top

AYUBU JELA MIAKA 30 KOSA LA KUBAKA MWANAFUNZI

16 August 2024
Share

Ayubu Teksi (26), Mkazi wa Kijiji cha Mgimba, Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka mtoto mwenye umri wa miaka 16, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza huko katika Kijiji cha Mgimba, Kata ya Gumanga, Tarafa ya Nduguti, Wilaya ya Mkalama.   

Mshtakiwa alikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa Mahakamani Juni 11, 2024 ambapo kutokana na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri kuiridhisha Mahakama, Mshtakiwa alipatikana na hatia, hivyo Mahakama kupitia Mhe.Luzango Omero Khamsini, Hakimu Mkazi Wilaya ya Iramba, akamuhukumu Mshitakiwa kwenda jela miaka 30.

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama, ili iwe fundisho kwa Mshtakiwa na kwa jamii kwa lengo la kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.