
Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Bundu Ngha’bi (32) mkazi wa kijiji cha Mwantemi, wilayani Itilima mkoani Simiyu amekutwa amejinyonga juu ya mti nje ya nyumba yake huku watoto wake wawili mmoja mwenye umri wa miaka miwili na mwingine miaka minne wakikutwa wamenyongwa katika chumba cha wazazi wao.
Kufuatia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Edith Swebe ametoa wito kwa wananchi kusaidia kutoa taarifa za kificho kwa jeshi hilo, iwapo mtu atapata taarifa kuhusu tukio hilo, ambalo hadi sasa mke wa marehemu hajulikani alipo.
