Back to top

Baba amjeruhi binti yake wa miaka 9 wakati akijaribu kumchinja.

19 November 2020
Share

Mwanaume mmoja mkazi wa Gairo mkoani Morogoro mwenye umri wa miaka 38  amekamatwa na polisi akituhumiwa kumjeruhi binti yake mwenye umri wa miaka tisa mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Kibedya akijaribukumuua kwa kumchinja kutokana na imani za kishirikina ili ajipatie mali.

Mwanaume huyo, Yakobo Taolo, 38 mkazi wa kitongoji cha Mabatini wilayani Gairo, anadaiwa kujaribu kumuua binti yake, Christina Yakobo,9, mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Kibedya,aliyelazwa hospitali kwa matibabu, tukio lililothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Wilbroad Mutafungwa.

SACP Mutafungwa akabainisha kuwa mke wa mtuhumiwa alisikia kelele za watoto na kukimbilia eneo la tukio alimkuta binti yao akivuja damu, na alipokuwa akitaharuki, mumewe alimkamata mwanamke huyo na kuanza kumnyonga ndipo wananchi wakajitokeza na kumshambulia baba huyo kwa kipigo na akafariki dunia akipatiwa matibabu.

Polisi wanamshikilia Robert Chidaka anayedaiwa  kumpeleka mwanaume huyo kwa mganga wa kienyeji.