Mtoto Fitina Tukolyese mkazi wa Tunduru mkoani Ruvuma amefariki kwa kuungua moto huku babu yake aitwaye Greyson Mtendele akijeruhiwa na kulazwa katika kituo cha afya Nakapanya baada ya kujitosa kwenye moto kumuokoa mjukuu wake bila mafanikio huku nyumba saba zikiteketea kwa moto na kuwaacha wakazi 33 kukosa mahala pa kuishi.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Simon Maigwa Marwa amesema mtoto Fitina Fadhil Tukolyese mwenye miaka miwili na miezi mitano amefariki kwa kuungua moto katika kijiji cha Mkowela alikomtembelea babu yake mzee Mtendele ambaye amejeruhiwa kwa moto wakati akijaribu kumuokoa mjukuu wake huyo.