
Bunge limepitisha bajeti ya Wizara ya ujenzi ya shilingi trilioni 1.77 iliyowasilishwa hapo Jana kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele tisa kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja, vivuko, mizani na ukamilishaji viwanja vikubwa vya ndege.
Katika wasilisho lake, Waziri Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, alisema katika mwaka huo wa fedha, Wizara inatarajia kutekeleza Mpango na Bajeti kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26).
Akijibu hoja za wabunge, Waziri Bashungwa amesema fedha yoyote itakayopelekwa Wizara ya Ujenzi itatumiwa kwa malengo ya kuwasaidia Watanzania kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na Mvua na kuwa hakutakuwa na ukwanguaji wa Barabara ambao mwisho wake hautakuwa na tija.
