Back to top

BAKWATA yatoa maagizo kwa shule za kiislamu nchini.

16 September 2020
Share

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA limetoa maagizo kwa wamiliki wote wa shule na viongozi wao kuchukua tahadhari ya uboreshaji miundombinu ya shule pamoja na ulinzi huku likiwasihi wananchi  na waislamu wote kuwa na subira wakati vyombo vya usalama vikiendelea na uchunguzi wa chanzo cha kuungua moto kwa shule za kiislamu.

Maagizo hayo ya BAKWATA yametolewa na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir ikiwa siku chache tu tangu kutokea kwa tukio la kuungua moto kwa shule ya msingi Byamungu ilioko mkoani Kagera wilaya ya Kyerwa na kusababisha vifo vya wanafunzi 10 na majeruhi.

Mufti wa Tanzania Shekh Abubakar Zubeir ametoa pole kwa mkuu wa shule  familia,serikali na wote walioguswa na msiba huo.