Back to top

Balozi John Kijazi ateuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

21 August 2020
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Balozi John William Herbert Kijazi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mhe. Balozi Kijazi ni Katibu Mkuu Kiongozi.

Uteuzi huu unaanza leo tarehe 21 Agosti, 2020.

Mhe. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Hayati Benjamin William Mkapa.