
Wadau wa Uchaguzi wametakiwa kuwa Mabalozi wazuri na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lakini pia kuzingatia sheria za uchaguzi, kanuni za Uboreshaji na maelekezo ya Tume kuhusu zoezi hilo.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Balozi Omar Mapuri wakati akifunga Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na wadau wa Uchaguzi uliofanyika mkoani Manyara.
Mkutano huo ni sehemu ya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura zoezi linalotarajiwa kuanza mkoani humo tarehe 4 Setemba hadi tarehe 10 Septemba, 2024.
“Pia napenda kuwaomba wadau wa uchaguzi kwa umoja wenu, kuzingatia sheria za uchaguzi, kanuni za Uboreshaji na maelekezo ya Tume kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari” alisema Mhe.Balozi Mapuri.
