Back to top

BARA LA AFRKA LINA UWEZO WA KUZALISHA CHAKULA CHA KUTOSHA

07 September 2023
Share

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, amesema Bara la Afrika lina uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha na kuuza nje ya Bara la Afrika kwani bara hilo limejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi za kilimo hivyo wananchi na viongozi wa bara hilo hawana sababu ya kuwa na unyonge wa kuthubutu kuongeza nguvu ya uwekezaji katika sekta muhimu ya kilimo na mifugo.

Rais Samia ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika, ambao umehudhuriwa na wakuu wa   mbalimbali kutoka nchi za Bara la Afrika ikiwa leo ni siku ya wakuu wa nchi kujadili mustakabali wa uzalishaji wa chakula chakutosha kwa nchi za Afrika.

Aidha Rais Samia ametoa rai kwa nchi za Afrika kuongeza juhudi za kuboresha bajeti za sekta ya kilimo katika kuendeleza mapinduzi ya kilimo kwa karne ya hii 21.

Akizungumza katika mkutano huo wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika, Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe.Evarist Ndaishimie amesisitiza umuhumu wa kuongeza msukumo wa maendeleo ya kilimo kwa vijana huku Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe.William Rutto mkutano huu wa Jukwaa la Chakula Afrika, unafanyika muda muafaka kwa nchi za Afrika.