Back to top

Barabara kufungwa kuelekea 'Royal Tour' Arusha.

27 April 2022
Share

Serikali Mkoani  Arusha, imewaarifu wananchi wa mkoa huo kuwa baadhi ya barabara zitafungwa kuanzia saa tano asubuhi, kupisha zoezi la uzinduzi wa Filamu ya Tanzania  'Royal Tour' Aprili 28 mwaka 2022, unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC), kuanzia majira ya saa nane mchana.


Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella, amesema hayo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC), alipokuwa anatoa taarifa kwa umma, kuhusu hatua iliyofikiwa katika matayarisho ya uzinduzi wa filamu hiyo ambayo dhana yake ni kutia chachu sekta ya utalii nchini.

Katika hatua nyingine amebainisha kuwa wageni 5,000 wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo na kwamba taratibu za kuingia (AICC), zitafanyika katika Hoteli ya Mount Meru.