Back to top

BASHE ATOA ONYO KWA HALMASHAURI

06 July 2023
Share

Waziri wa Kilimo, Mhe.Hussein Bashe, ametoa onyo kwa Halmashauri za Wilaya nchini, kuacha mara moja tabia ya kunyemelea maeneo ya  ardhi ya mashamba ya uzalishaji wa mbegu na yale ya utafiti na kutaka kugeuza matumizi kwa kuyafanya viwanja kwa ajili ya ujenzi kwa kuzingatia umuhimu wa meneo hayo kwenye maendeleo ya kilimo nchini.

Waziri Bashe ametoa onyo hilo Mkoani Arusha, wakati wa ziara yake kwenye Taasisi ya uzalishaji wa Mbegu Nchini, kwa lengo la kuona maendeleo ya uzalishaji wa mbegu nchini.

Amesema Serikali inamkakati wa kukabilina na tatizo la upungufu wa zao la ngano hapa nchini.