Back to top

Bashungwa atoa maagizo kwa Maafisa Elimu.

14 January 2022
Share

Waziri wa TAMISEMI Mh. Innocent Bashungwa amewaagiza maafisa wa elimu wa mikoa na Wilaya, nchini kuwasimamia wakuu wa shule, walimu wakuu na walimu wa masomo, kuzingatia kalenda ya utekelezaji wa mitaala ili kuwa na ufundishaji na ujifunzaji wenye tija.
.
Waziri Bashungwa ametoa maagizo hayo wakati akizindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule, Jijini Dodoma.