Back to top

BASHUNGWA ATOA SAA TATU BARABARA MBADALA IPATIKANE

04 March 2024
Share

Waziri wa Ujenzi Mh.Innocent Bashungwa, ametoa saa tatu kwa Wakala wa Barabara (TANROADS) kuhakikisha wanarejesha mawasiliano ya barabara ya Mtwara-Mingoyo-Masasi, ambayo yamekatika baada ya daraja lililopo eneo la Maili Mbili, kusombwa na maji, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. 
.
Bashungwa ametoa agizo hilo wilayani Masasi, akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mh.Deo Ndejembi, walipofika katika eneo hilo ambalo watumiaji wa barabara walikwama tangu Asubuhi.
.
“Natoa saa tatu kwa TANROADS kuhakikisha inakamilisha kujenga barabara ya mbadala ili magari na wananchi waanze kupita", Waziri Bashungwa.
.
Naye, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Deo Ndejembi amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 30 zimetolewa na Rais kwa ajili ya dharura za matengenezo ya barabara nchi nzima kupitia Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).