Back to top

Bashungwa atoa siku 7 uchunguzi soko la Karume.

16 January 2022
Share

Waziri wa TAMISEMI Mh. Innocent Bashungwa ametoa siku saba kwa Tume iliyoundwa kuchunguza kuungua kwa soko la Karume Jijini Dar es Salaam kuhakikisha imekamilisha uchunguzi wake ili wafanyabiashara hao waweze kuendelea na shughuli zao za kujitafutia kipato huku akiwaagiza Wakuu wa Mikoa kote nchini kufanya tathmini ya athari za moto kwenye wilaya zote na kuleta taarifa ndani ya siku 14 ili kuwe na mipango thabiti ya kuzuia ajali za moto kwenye maeneo yote.