Back to top

BASHUNGWA: MKANDARASI ALIYEDHULUMU ATAFUTWE

29 February 2024
Share

Waziri wa Ujenzi, Mhe.Innocent Bashungwa, amemuagiza Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), kumtafuta na kumchukulia hatua za kisheria, Mkandarasi Mohammed Ally, wa Kampuni ya Sure Civil and Building Contractors Company Limited, aliyetekeleza ujenzi wa majengo katika Hospitali ya wilaya Karagwe ‘Nyakanongo’ kwa kushindwa kulipa shilingi Milioni 24.7/= ya vifaa vya ujenzi alivypokopa kwa mfayabiashara licha ya ujenzi huo kukamilika miaka miwili iliyopita.
.
Bashungwa ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea malalamiko hayo kutoka kwa Mfanyabiahara, Abineza Ginivian wakati akikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mji wa Kayanga, uliopo wilayani Karagwe.
.
Akiongea kwa njia ya simu na Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Rhoben Nkori, Waziri Bashungwa amemuagiza kumtafuta Mkandarasi huyo kuhakikisha analipa deni ambalo alikopa kwa mfanyabiashara huyo wakati ujenzi wa hospital ya wilaya Karagwe ukitekelezwa.
.
Abineza Ginivian, ameeleza kuwa baada ya kumkopesha vifaa ya ujenzi Mkandarasi huyo, amekuwa akimzungusha na kukata mawasiliano, na baada ya kumfuata ofisini kwake mkoani Dar es Salaam alikana deni hilo la milioni 24.7/=.