Back to top

Basi la Isamilo lapinduka na kujeruhi 22, wa nne hali zao mbaya.

10 September 2020
Share

Watu 22 wamejeruhiwa na kati yao wanane hali zao ni mbaya baada ya basi la kampuni ya Isamilo Express walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Mbeya kwenda Mwanza kuacha njia na kupinduka katika eneo la Inyala mkoani Mbeya.

Ajali hiyo imetokea leo katika eneo la Inyala umbali wa takriban kilometa 20 kutoka katikati ya jiji la Mbeya wakati basi hilo la kampuni ya Isamilo likiianza safari kuelekea jijini Mwanza.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi, Ulrich Matei akaeleza chanzo cha ajali hiyo huku akitoa rai kwa madereva kuwa waangalifu.