Back to top

Basi la kampuni ya Emigrace laua 7 lajeruhi 30 Kondoa.

02 October 2021
Share

Watu 7 wamefariki na wengine 30 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Emigrace walilokuwa wakisafiri kutoka Babati kuelekea jijini Dar es Salaam lenye namba za usajili T 703 DLG kupinduka katika mlima Kolo wilayani Kondoa mkoani Dodoma.
.
Taarifa ya awali ya polisi imesema chanzo cha ajali hiyo ni breki za gari kushindwa kufanya kazi hali iliyomsinda dereva kuliongoza na kisha kupinduka mtaroni.
.
Majeruhi wamepelekwa hospitali za wilaya za Kondoa na Babati na miili yote imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kondoa.
.
Dereva wa basi hilo amekimbia mara baada ya ajali na juhudi za kumtafuta zinaendelea.