
Watu wanne wamejeruhiwa baada ya basi la Shabiby lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma, kupinduka katika eneo la Kihonda kwa Chambo, barabara kuu ya Morogoro - Dodoma, wakati dereva akijaribu kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake na kukutana na bajaji na alipojaribu kuikwepa ndipo basi hilo likaanguka.
Ajali hiyo imehusisha basi lenye namba za usajili T.341 EEU, ambapo baadhi ya abiria waliokutwa eneo la tukio wamesema chanzo cha ajali ni dereva wa basi kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari ambapo katika kukwepa bajaji ndipo gari ikamshinda na kuanguka.

Jitihada zaidi kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro bado zinaendelea baada ya kuelezwa yuko kwenye mazoezi yanayoshirikisha majeshi mbalimbali.
