Back to top

BAWACHA wataka wabunge 19 viti maalum wasitambulike bungeni.

04 May 2021
Share

Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) limetoa rai kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kusimamia misingi ya katiba ya nchi kwa  kutowatambua wabunge wa viti maalum 19 waliofukuzwa uanachama na chama hicho pamoja na  kujibu barua ya chama iliyowasilishwa bungeni hapo kwa taratibu za kiofisi.


Baraza la Wanawake  CHADEMA limesema utaratibu uliofanywa na chama hicho katika kuwavua uanachama  wabunge hao 19 na  kuwasilisha barua ya hatua hiyo ulizingatia katiba ya chama huku  baraza hilo likihoji ukinzani wa taarifa inayotolewa na Spika Ndugai pamoja na naibu spika tulia akson juu ya kupokelewa barua ya chama hicho.


Hatua ya BAWACHA kutoka hadharani na kuzungumza na vyombo vya habari imejiri mara baada ya Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Job Ndugai kukosoa barua ya CHADEMA iliyowasilishwa kwenye ofisi yake kuhusu kuvuliwa uwanachama wabunge hao wa viti maalum wapatao 19.