
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta, huku ikibainisha kuwa bei za rejareja na jumla za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa nchini zimebadilika ikilinganishwa na toleo la Februari 02, 2022 ambapo kwa mwezi Machi bei za rejareja kwa petroli na dizeli zimeongezeka kwa Tsh. 60/= kwa Lita (sawa na 2.42%) na Tsh. 65/= kwa lita (sawa na 2.77%) huku mafuta ya taa yakipungua kwa Tsh. 83/= kwa lita (sawa na 3.63%).
