Back to top

Beki wa Yanga SC Lamine Moro kukosa mechi 3.

25 June 2020
Share

Kamati ya saa 72 iliyoketi June 23 imemfungia beki wa Yanga Lamine Moro mechi 3 na kumpiga faini ya shilingi laki 5 kwa kosa la kumrukia mgongoni hadi kuanguka chini mchezaji wa JKT Tanzania Mwinyi Kazimoto katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma June 17.

Aidha Mwinyi Kazimoto naye amepewa adhabu ya kukosa mechi mbili kwa kosa la kuleta vurugu uwanjani katika mechi hiyo.