Back to top

Benard Morrison aibukia Msimbazi na kusaini Mkataba.

08 August 2020
Share

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Benard Morrison ametua msimbazi na kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo, ambapo ameonekana ametinga uzi wa wekundu wa msimbazi Simba huku akionekana mwenye bashasha.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Simba SC walipakia picha tatu zikimuonesha Morrison akisaini dili hilo ambalo linahisiwa huenda likawa la mika miwili licha kuwa Simba wenyewe hawakuweka wazi kuwa dili hilo ni lamiaka mingapi.

Usajili huu unakuwa wa kwanza kwa Simba kutambulishwa rasmi kwa ajili ya msimu wa 2020/21, hata hivyo thamani ya dau lake inatajwa huenda ikawa ni kama zaidi ya milioni 150.   

Picha za Morrison