Back to top

Benki ya dunia kuiongezea Tanzania fedha za kupambana na umaskini.

09 June 2021
Share

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya dunia kanda ya Afrika Dkt.Taufila Nyamadzabo amesema benki hiyo imeridhishwa na Tanzania kufanya vizuri katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini(TASAF), kutokana na kutekeleza mpango huo vizuri tofauti na nchi ya Sudan na Sudan Kusini ambazo ametembelea na kuahidi kuongeza fedha katika utekelezaji wa mpango huo.
.
Dkt .Nyamadzabo amesema hayo Jijini Dodoma wakati alipotembela baadhi ya wanufaika wa TASAF ambapo amesema Tanzania imeonyesha muelekeo mzuri katika utekelezaji wa mpango huo kutokana na walengwa wengi kuonyesha kujiinua kiuchumi.
.
Aidha, Mkurugenzi wa TASAF Ladisilaus Mwamanga amesema zaidi ya vijiji 10,000 vimeweza kufikiwa na Mpango wa Kunusuru  Kaya Maskini (TASAF) unaotekelezwa kwa ajili ya kuwakwamua wananchi ili waondokane na umaskini.