Back to top

Benki ya Dunia yakoshwa na utekeleza wa Ujenzi wa Reli Tanzania.

24 August 2019
Share

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, Bi.Anne Kabagambe, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutekeleza Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) kwa kutumia fedha zake za ndani.

Bi.Kabagambe anayewakilisha nchi 22 za Kanda ya Afrika katika Benki hiyo yenye Makao yake Makuu Washington DC nchini Marekani, ametoa kongole hiyo kwa Rais Dokta John Magufuli, baada ya kutembelea na kukagua sehemu ya ujenzi wa miundombinu ya reli hiyo, kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro.

Kadhalika ameahidi kuwa wakati Benki ya Dunia ikiangalia namna ya kuongeza ufadhili wa miradi kwa Tanzania, ataishawishi Benki hiyo pamoja na  taasisi nyingine za Kimataifa zinazotoa misaada na mikopo kutoa fedha ili Tanzania iweze kutimiza malengo yake ya kukamilisha ujenzi wa Reli hiyo ambayo itafungua fursa za kiuchumi ukanda wa Afrika.

Mkurugenzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Reli, Kutoka Kampuni ya Reli-TRC, Mhandisi Felix Nlalio amesema ujenzi wa reli hiyo unaokwenda kwa kasi ili uweze kukamilika kwa wakati na kuiletea faida nchi.

Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa unaohusisha awamu mbili, Kipande cha kwanza kati ya Dar es Salaam na Morogoro na kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuongeza mapato katika Bandari ya Dar es Salaam na kutaimarishara biashara hususani kati ya Tanzania na nchi zinazopitiwa na ushoroba wa kati za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda na Rwanda.