
Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote, umewasilishwa Bungeni Jijini Dodoma, ambapo kutokana na upekee wa Mfuko huo, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha zimependekeza baadhi ya vyanzo vya mapato kuendesha mfuko huo.
.
Vyanzo hivyo ni pamoja na sehemu ya mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa zenye Cabon (Cabonated Drinks), vinywaji vikali(Liquor), bidhaa za vipodozi (Cosmetics Product), Michezo ya kubahatisha, ada ya bima za vyombo vya moto na mapato yatokanayo na miamala ya mifumo ya kielektroniki kwa kadri itakavyopendekezwa na Waziri mwenye dhamana na masuala ya Fedha, fedha zitakazotengwa na Bunge, mapato yatokanayo na uwekezaji wa mfuko na zawadi
pamoja na misaada kutoka kwa wadau mbalimbali.
.
Waziri Ummy ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Muswada huo, ambao ulikwama mwezi Februari mwaka huu kwa hoja iliyotolewa na Bunge ya kutokuwepo kwa chanzo endelevu cha fedha za kutekeleza mpango huo.