Back to top

BIDEN KUTUA ISRAEL KUTETA NA NETANYAHU

17 October 2023
Share

Rais wa Marekani Joe Biden, anatarajiwa kufanya ziara nchini Israel kesho Jumatano, ambapo anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu, mazungumzo yanayolenga kuithibitishia nchi hiyo juu ya uungaji mkono katika kuhakikisha usalama wa Israel.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameeleza juu ya ziara ya Rais Biden huku akisisitiza kuwa Biden atathibitisha tena uungwaji mkono thabiti wa Marekani kwa Israel na kujitolea kwa nchi hiyo kwa ajili ya usalama wa Israel.

Blinken amesema Israel ina haki na wajibu wa kuwalinda raia wake dhidi ya Hamas na makundi mengine ya kigaidi na kuzuia mashambulizi ya siku za usoni.