Back to top

Bidhaa zisizokuwa na ubora zenye nembo ya “TBS” zauzwa mtaani Ruvuma

03 December 2019
Share

Wafanyabiashara na wananchi mkoani Ruvuma wamelalamikia bidhaa zisizokuwa na viwango kuuzwa mitaani zikiwa  na nembo ya shirika la viwango Tanzania (TBS) na kuitaka mamlaka hiyo kuwa makini ili kulinda afya za walaji.
 
 
Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na  viongozi wa shirika la viwango Tanzania na kuitaka mamlaka hiyo kuongeza umakini kuanzia viwandani zinakotengenezwa bidhaa badala ya kuwasumbua wauzaji ilhali bidhaa ina nembo ya TBS
 
Ili kuondoa malalamiko ya wananchi kulalamikia kuathirika kiafya kutokana na kutumia bidhaa zisizokuwa na viwango afisa viwango wa TBS Bi. Fatuma Mauniko  amewataka wananchi kushirikiana na shirika hilo ili kuondoa bidhaa zisizokuwa na viwango.

Kwa upande wake mwakilishi wa kaimu mkurugenzi wa  udhibiti ubora wa TBS Bw.Hamis Sudi Mwanasala amewataka wauzaji kuuza bidhaa zilizothibitishwa na TBS ili kulinda afya za walaji.