Back to top

BIL 97 KUJENGA BARABARA IFAKARA-MBINGU

16 May 2024
Share

Kukamilika kwa ujenzi wa barabara itakayojengwa kwa kiwango cha lami  kutoka Ifakara hadi Mbingu yenye urefu wa kilomita 62.5 kwa gharama ya Bilioni 97.178 unatarajia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo za kilimo.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Igima, kijiji cha Lufufu Wamesema kukamilika kwa ujenzi wake kutapunguza gharama za usafiri na usafirishaji wa mazao hayo kwenda kwenye masoko ya mjini na kuongeza thamani ya mazao ya wakulima fofauti na sasa kutokana na kuwepo changamoto za miundombinu ya barabara.

Akizungumza mara baada ya kukagua hatua zinazoendelea za kuanza ujenzi wa barabara hiyo, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba amesema kuwa kilio kikubwa cha wananachi ni kupata barabara ya lami na tayari imetoa fedha na mkandarasi yupo eneo la mradi, kwa ajiili ya ujenzi huo.

Mhandisi Kyamba amesema kuwa mradi huo utasimamiwa na kitengo cha usimamizi wa miradi cha TANROADS (TECU) na ni wa miezi 30 ambao umeanza tarehe 8 Disemba 2023 na unatarajiwa kumalizika ifikapo tarehe 8 Juni 2026.