
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema wametenga kiasi cha shilingi bilioni 5 katika mwaka wa fedha 2023/2024, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Magharibi ambapo ujenzi utaanza na jengo la huduma za wagonjwa wa nje (OPD).
.
Dkt.Mollel ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Malum, Mhe. Zainabu Athumani Katimba, aliyeuliza ni lini Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi itaanza kujengwa, .
.
Dkt. Mollel amesema kuwa ujenzi huo utaanza mapema mwezi Januari 2024 ili wananchi wa Kanda ya Magharibi na mikoa jirani waweze kupata Huduma za afya kwa wakati.
