Back to top

Bilioni 100 zatengwa kupambana na bei ya mafuta.

10 May 2022
Share

Serikali imetoa shilingi bilioni 100  kwa ajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini fedha ambazo zitatolewa katika matumizi ya serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha uliobaki kwa mwaka 2021/2022 na fedha hizo hazitagusa miradi  ya maendeleo inayoendelea.

Hayo yamesemwa bungeni na Waziri wa Nishati Mhe January Makamba alipokuwa akitoa taarifa bungeni kuhusu mikakati  ya serikali ya  kupunguza bei za mafuta nchini.

Akaongeza kuwa fedha hizo zitaanza kutumika Juni mosi mwaka huu kwani kwa  sasa hawawezi kuanza kufanya hivyo kutokana na wauzaji na   wanunuaji wa mafuta tayari wameshanunua mafuta kwa bei inayotumika sasa.

Makamba akaongeza kuwa katika kuhakisha bei za mafuta zinapungua kwa sasa serikali imeruhusu pia watu wengine wanaoweza kuingiza mafuta kutoka nje wafanye hivyo ili kupata unafuu.