Back to top

BILIONI 113 KUJENGA BARABARA YA ZEGE KUELEKEA LIGANGA NA MCHUCHUMA.

24 January 2024
Share

Serikali imesema imeanza kutekeleza ujenzi wa barabara ya Itoni-Lusitu (km 50) kwa kiwango cha zege, ambayo itagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 113 ili kurahisisha usafirishaji wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na madini ya Chuma cha Liganga.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa Wilayani Ludewa mara baada ya kukagua barabara hiyo pamoja na kipande cha Lusitu-Mawengi (km 50) kilichokamilika kwa kujengwa kiwango cha zege na Wananchi tayari wameshaanza kunufaika nayo.

Vilevile, Waziri Bashungwa amemtaka Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara Itoni – Lusitu (km 50), Cheil Engineering Co. ltd kumsimamia kwa karibu mkandarasi China Civil Engineering Construction Cooperation ili aweze kukamilisha mradi huo Disemba 2024 kama mkataba unavyosema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kutoa bilioni 15 kwa kulipa fidia wananchi waliopisha miradi hiyo ya mchuchuma na liganga.