Back to top

Bilioni 1.9 kulipa fidia wananchi kupisha hifadhi ya bonde mto Ruhila

07 April 2022
Share

Serikali Wilayani Songea mkoani Ruvuma imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 1.9 kulipa fidia wananchi kupisha hifadhi ya bonde la mto Ruhila ambalo linatunza maji yanayolisha mji wa Songea hivyo serikali imepiga marufuku wananchi kulima kwenye bonde hilo.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw.Pololeti Mgema kwenye upandaji wa miti katika bonde hilo huku akiwataka wananchi wanaoendelea kulima kwenye bonde hilo kuacha mara moja.

Mkuu wa shule ya wavula ya Songea ambao ni majirani na shule hiyo Mwalimu John Sweke amesema atatoa ushirikiano wa kulilinda na kutunza miti inayopandwa kwenye bonde hilo kusaidia ulindaji nauhifadhi wa mazingira.

Afisa misitu wa Manispaa ya Songea Bw.Godfrey Luhimbo amesema wanapanda miti kwenye bonde hilo kwa kuwa lina umuhimu mkubwa kwa wananchi wa manispaa hiyo.