Back to top

Bilioni 200 zatengwa ununuzi wa dawa na vifaa tiba

11 November 2022
Share

Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba katika mwaka wa fedha 2022/2023 huku Bilioni 74.3 zikiwa tayari zimetolewa katika kumaliza changamoto ya upungufu wa dawa na vifaa tiba nchini.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel leo Novemba 11,2022 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Mhe.Ghati Zephania Chomete, katika kikao cha kumi cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jijini Dodoma.

"Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga bajeti ya shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba na hadi kufikia tarehe 30 Oktoba, 2022 Serikali imekwisha toa jumla ya shilingi bilioni 74.3 kwa ajili ya manunuzi ya dawa na vifaa tiba ili kuimarisha upatikanaji wake katika ngazi zote za utoaji wa huduma za Afya." Amesema Dkt. Mollel. 

Aidha, amesisitiza kuwa, Serikali itaendelea kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya nchini kwa kuboresha miundombinu ikiwemo kuweka vifaa tiba vya kisasa, kuajiri Wataalamu wa Afya pamoja na kuwapandisha madaraja ili kuongeza morali ya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.