Back to top

Bilioni 2.8 zatolewa kufanikisha mradi wa maji Namanga.

23 July 2020
Share


Serikali imetoa shilingi bilioni 2.8 ili kufanikisha mradi wa maji katika mji wa Namanga wilayani Longido mkoani Arusha.

Taarifa za utekelezaji wa mradi huo zimetolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw.Iddy Kimanta alipokuwa anajibu malalamiko ya wananchi wa mji wa Namanga wanaokabiliwa na tatizo kubwa la maji.

Awali akikagua mradi wa ujenzi wa hosipitali Bw.Kimanta amewataka watendaji wa wilaya hiyo kuhakikisha fedha za miradi zinazotolewa na serikali zinapelekwa kwenye miradi husika kwa wakati.

Pamoja na malalamiko ya wananchi wa Longido kwa sasa baadhi ya miradi inayotekelezwa imeanza kutatatua baadhi ya kero ikiwemo ya maji na pia upatikanaji wa huduma za kijamii zikiwemo za afya.

Mkuu wa mkoa Bw.Kimanta yuko katika ziara ya kukagua miradi na kusikiliza kero za wananchi.