Back to top

Bilioni 4 zatengwa ununuzi vifaa vya kuchakata mazao.

20 April 2021
Share

Wizara ya viwanda na Biashara imetenga shililingi bilioni 4  kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya ununuzi wa mashine ndogo na kisasa za kuzalisha na kuchakata mazao ya wakulima kupitia Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini (SIDO).

Hayo yamebainishwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa viwanda na biashara Mh Xaud Kigahe wakati akijibu swali la Mbunge wa Vunjo Mh Charles Kimei aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani kupitia SIDO kutengeneza mashine zitakazosaidia kuchakata mazao ya wakulima ambao mazao yao yamekuwa yakiharibika shambani na sokoni kwa kukosekana viwanda vya kuchakata mazao hayo.

Mh Kigahe amesema mpango huo utakwenda sawia na utoaji wa elimu kwa wajasiriamali wadogo namna ya kutambua umuhimu wa mashine hizo wakati wa kuzitumia na kuwa na tija kwa kuwapatia mapato baada ya kuchakata mazao yao kupitia mashine hizo zitakazokuwa zinatengenezwa SIDO kote nchini.