Back to top

BILIONI 9 ZATOLEWA KWA AJILI YA MAFUNZO FANI ZA UBINGWA. 

26 August 2023
Share

Serikali imetoa fedha kiasi cha Tsh.Bil. 9, kwa ajili ya mafunzo ya wataalamu wa Afya katika fani za za ubingwa na ubingwa bobezi, Ili kusaidia  kukabiliana na changamoto ya upungufu wa fani hizo katika maeneo ya utoaji huduma za afya kwa wananchi. 
.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, wakati akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu mpango wa kila mwaka wa ufadhili wa masomo kwa Wataalamu wa afya katika kada mbalimbali unaojulikana kama "Samia Suluhu Super Specialists Program".
.
Aidha, Dkt.Mollel amebainisha kuwa mageuzi makubwa yanazidi kufanyika ndani ya Sekta ya afya lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za matibabu.