Back to top

BIMA AFYA KWA WOTE, SULUHU YA MATIBABU BURE KWA WAZEE

02 April 2024
Share

Serikali imesema Bima ya Afya kwa wote itakuwa suluhu ya kudumu ya utekelezaji wa Sera ya wazee kupata matibabu bure katika kila Kituo cha Afya nchini.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, wakati akijibu swali kutoka kwa Mbunge wa Viti Maakum Mhe. Tauhida Cassian Gallos aliyeuliza, Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha Sera ya Wazee kupata matibabu bure inatekelezwa katika kila Kituo cha Afya nchini.
.
Amesema, wazee wasio na uwezo wa kugharamia huduma za Afya wameendelea kupatiwa huduma hizo kwa utaratibu wa msamaha huku akikili kuwa ni kweli kuna changamoto kwenye baadhi ya maeneo, ambapo ametoa wito kwa wabunge na madiwani kuhakikisha wanashirikiana ili kusimamia Sera ya Wazee kupata matibabu bure inatekelezwa katika maeneo yao.