Back to top

BINTI WA RAIS WA ZAMANI WA ANGOLA KUKAMATWA

30 November 2022
Share

Serikali ya Angola imetoa hati ya kumkamata, Isabel dos Santos, binti wa Rais wa zamani wa nchi hiyo José Eduardo dos Santos, kwa madai ya kutumia vibaya madaraka na ubadhirifu wa fedha za umma.

Shirika la habari la Angola, limevinukuuu vyombo vya habari vya serikali vikisema Mwanasheria Mkuu wa Angola, Hélder Pitta Gróz, akisema Isabel dos Santos, anatafutwa kwa kesi kadhaa za jinai.

Isabel dos Santos, mwenye umri wa miaka arobaini na tisa, anayeaminika kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika, aliwahi kuwa mkuu wa kampuni ya mafuta ya Sonangol. Anakabiliwa na kesi ya ufisadi ya dola bilioni tano lakini ameakanusha madai hayo.