Back to top

BITEKO ATANGAZA KUWAONDOA MAMENEJA WAZEMBE TANESCO

04 April 2024
Share

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko ametangaza oparesheni maalumu ya kuwaondoa Mameneja wote wa TANESCO wa Mikoa, ambao watabainika kushindwa kutatua matatizo yanayoripotiwa na wateja kwa wakati.
.
Mhe.Biteko ameyasema alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha miito ya simu cha huduma kwa wateja TANESCO Ubungo, mkoani Dar es Salaam, ambapo ameagiza kila Mkoa nchini, uliopo chini ya TANESCO ufanyiwe tathmini ili kujua umeme umekatika mara ngapi na sababu zilizosababisha umeme kukatika kwenye maeneo hayo ili kama ni uzembe umefanyika Serikali iweze kuchukua hatua haraka.
.
Aidha, Dkt. Biteko ameagiza, kituo kuangalia utaratibu wa namna nzuri ya wateja kutogharamia malipo kipindi wanapopiga simu kuhudumiwa na kituo.