Back to top

BITEKO ATOA MAELEKEZO KWA Ma-DC, Ma-DAS NA Ma-DED

09 May 2024
Share

Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmshauri nchini wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo ili kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akifungua warsha ya Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za mikoa tisa ya Tanzania Bara kuhusu Usimamizi na Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai iliyofanyika Jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa mada mbalimbali zitawasilishwa na wabobezi kutoka sekta tofauti, hivyo walengwa wajipange kupata maarifa na kuzingatia yote watakayoelekezwa katika warsha hiyo kwa ajili ya kuboresha utendaji wao wa kazi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Zainab Katimba amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Tume ya Haki Jinai na kuwa Ofisi yake ipo tayari kuhakikisha azma ya Rais Samia inafanikiwa.

Warsha hiyo kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri kutoka Tanzania Bara imehudhuriwa na washiriki kutoka mikoa tisa ya Arusha, Geita, Kilimanjaro, Mara, Simiyu, Shinyanga.