
Serikali imesema kuwa mgao wa umeme upo ukingoni kutokana na jitihada kubwa ambazo imekuwa ikizifanya, kukabiliana na changamoto ya Umeme ikiwa ni pamoja na kuwekeza fedha nyingi katika miradi mbalimbali ya Umeme.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko, leo Februari 23 ,2024 alipoambatana na Waziri wa maji, Mhe.Juma Aweso, kwenye ziara ya kukagua Bwawa la kuzalisha Umeme la Kidatu, ambapo amewataka Watanzania kuvumilia kidogo kwani changamoto hiyo inakwenda kuisha.
.
“Serikali ya Awamu ya sita ya Mhe Dkt Samiah Suluhu Hassan imeshatoa fedha nyingi kwajili ya kukabiliana na changamoto ya Umeme nchini, niwaombe wananchi kuvumilia kidogo, suala la mgao wa Umeme linakwenda kwisha!"Alisema Mhe.Biteko
.
Aidha, Mhe.Biteko amewaonya baadhi ya wananchi wenye tabia ya kuchepusha mito ya maji inayokwenda kwenye mabwawa ya kuzalishia umeme, kwa shughuli zao binafsi ikiwemo kilimo katika vyanzo vya maji, vitendo vinavyoharibu vyanzo vya maji.
.
Kwa upande wake Waziri wa Maji, Mhe.Jumaa Awessu, ameahidi kushirikiana na Wizara ya Nishati katika kutokomeza ukame, katika mabwawa ya kuzalishia Umeme, pamoja na kuhakikisha maji yanapatikana kwa wananchi wote.
