Back to top

BMH YAWEKA MLANGO WA BANDIA KWENYE MOYO

16 February 2024
Share

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), imefanikiwa kufanya upasuaji wa kuweka mlango wa bandia kwenye moyo, upasuaji ambao hufanyika pale mlango wa moyo (Valve) unapokuwa umeziba, na kuifanya Hospitali hiyo kuwa ya pili nchini kuanzisha huduma hiyo.
.
Akitoa taarifa hiyo Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo katika hospitali hiyo, Ahmed Toure, amesema mlango huo unapobadilishwa mgonjwa anapona tatizo lililokuwa linamsumbua la mlango kuziba na damu itapita vizuri kama zamani.
.
Upasuaji huo umefanyika kwenye kambi ya pamoja ya matibabu ya moyo kati ya madaktari wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na wenzao kutoka Uholanzi, iliyoanza Jumatatu, Februari 12, 2024 na inatarajiwa kukamilika leo Ijumaa Februari 16, 2024.