Back to top

Bobi Wine Avamiwa na wanajeshi nyumbani kwake.

12 January 2021
Share

Mgombea wa urais nchini Uganda Bobi Wine, amesema kwamba wanajeshi wamevamia nyumbani kwake na kukamata walinzi wake, zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu.

Msemaji wa polisi Kampala, Patrick Onyango, amekanusha madai hayo ya wanajeshi kuvamia nyumbani kwa Bobi Wine, akisema kwamba hakuna mtu aliyekamatwa, akielezea kwamba maafisa wa usalama wanaweka tu mikakati ya kiusalama katika sehemu zilizo karibu na nyumbani kwa Bobi Wine.

Bobi Wine pia ameambia waandishi wa habari kwamba mmoja wa madereva wake alipigwa risasi na wanajeshi Jumatatu, na akafariki jumanee asubuhi wakati akipata matibabu.

VOA