Back to top

BODABODA ENDELEENI KUFUATA SHERIA ILIYOPO - POLISI

28 July 2023
Share

Jeshi la Polisi Nchini limesema kuwa limepokea maswali toka kwa wanahabari na wananchi wa kada mbalimbali, wakitaka kujua msimamo wa Jeshi hilo, kufuatia matamshi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Bw.Abdulrahman Kinana, aliyoyatoa Julai 27,2023, akiwa kwenye mkutano wa hadhara, huko Bariadi, mkoani Simiyu, ambapo matamshi ya Kiongozi huyo, yalinikuliwa akisema watazungumza na kuishauri Serikali ili kupitisha sheria ya Bodaboda kubeba watu zaidi ya mmoja.
.
Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi hilo, SACP David Misime, amebainisha kuwa Jeshi hilo linasimamia sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo miongoni mwa sheria hizo ni kifungu namba 59 cha Sheria ya Usalama Barabarani Sura 168 ambacho kinakataza pikipiki kubeba abiria zaidi ya mmoja, ambapo amewaelekeza bodaboda wote nchini kufuata sheria iliyopo kwa sasa ambayo Jeshi hilo linaisimamia.