Back to top

Bodi ya korosho kuundwa upya ili kusimamia vema zao hilo.

22 March 2019
Share


Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga amesema katika kukabiliana na msimu huu wa kilimo, Bodi ya Korosho itaundwa upya ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa Mkurugenzi Mkuu wa kuiendesha ili kusimamia vema zao la korosho.

Amesema mbali na kuundwa kwa bodi hiyo, pia wizara itapitia mfumo uliyotumika kulipa wakulima wa korosho ili kubaini mafanikio na matatizo yaliyojitokeza ili yafanyiwe kazi.

Waziri Hasunga ameosema kuwa mambo mengine ni pamoja na kuhakikisha katika msimu huu baadhi ya viwanda vya korosho, ambavyo havifanyi kazi vinafufuliwa pamoja na kujenga viwanda vipya na kuwaomba viongozi wa halmashauri kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuwapatia ardhi kwa ajili ya kuwekeza viwanda.