
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetoa taarifa juu ya tathmini ya viwanja vilivyotumika kwa michezo ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2021/2022 ambapo imebaini mapungufu katika viwanja vya Mkwakwani (Tanga), Ilulu (Lindi), Ushirika (Kilimanjaro), Mabatini (Pwani), Sokoine (Mbeya), Jamhuri (Dodoma) na Nyankumbu Girls (Geita) yanayovifanya viwanja hivyo kukosa sifa ya kutumika kwa michezo ya Ligi hiyo msimu wa 2022/2023.
.
Hata hivyo Bodi hiyo imezitaka klabu zinazotumia viwanja hivyo kufanya maboresho ili kukidhi matakwa ya sheria zinazoongoza mpira wa miguu.

