Bodi ya nyama yapiga marufuku uchinjaji katika maeneo yasiyo rasmi.

Bodi ya nyama nchini imepiga marufuku kuchinja aina yoyote ya mnyama katika machinjio yasiyo rasmi ikiwemo minada ili kuepusha uwezekano wa upatikanaji wa magonjwa yanayoweza kutokea ikiwemo oma ya mapafu.

Kaimu Msajili wa bodi hiyo Imani Sichalise akizungumza jijini Dodoma alipokuwa akikagua machinjio ya kisasa ya Dodoma (TMS) amesema kuwa mtu yoyote atakayekamatwa akichinja nje ya machinjio yasiyotambulika na serikali atakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria ikiwemo nyama yake kutaifishwa.